CHRISTENSEN KUMKANDAMIZA WENGER LEO USIKU - Darajani 1905

CHRISTENSEN KUMKANDAMIZA WENGER LEO USIKU

Share This
Beki kisiki asiyependa kucheka na mtu anapokuwa kwenye majukumu yake, Andreas Christensen amesema maejiandaa vyema yeye pamoja na timu katika kumkandamiza na kumshindilia magoli mengi timu ya Arsenyani(Arsenal) iliyochini ya kocha Arsene Wenger leo usiku.

Beki huyo kisiki wa Chelsea ametioa neno hilo mara baada ya jana usiku kusaini mkataba mpya hapo jana ambapo amesaini mkataba wa miaka minne na nusu, alisema "Tuliangalia video ya mchezo uliopita ili kuona wapi tulifanya makosa, na tumeyagundua makosa yetu ambapo kosa mojawapo ilikuwa tunawaachia sana wapite. Lakini tulifika mazoezi na kujiweka sawa na kuyafanyia kazi makosa yetu na pia tumegundua ni jinsi gani tunaweza kuwaumiza. Wote tumejiandaa vyema na tupo tayari kupambana nao" alisema kinda huyo mwenye miaka 21.

Chelsea ilitoka suluhu katika mchezo uliopita dhidi ya Arsenyani kwa suluhu ya 2-2 ingawa kama nafasi zilizopatikana zingetumika vizuri, basi Chelsea ingepata alama hizo tatu muhimu huku kwa upande wa Christensen akiendelea kuwa na kiwango bora zaidi kwa kuwa kati ya walinzi makinda wenye uwezo mkubwa na huku akiziba vyema pengo la David Luiz.

No comments:

Post a Comment