Leo usiku kutakuwa na mchezo muhimu wa hatua ya nusu fainali ya kombe la Carabao, ambapo Chelsea itaikaribisha Arsenyani(Arsenal) uwanjani Stamford Bridge kucheza mchezo mara baada ya kupita wiki moja tu toka kumenyana katika mchezo wa ligi kuu ambao uliisha kwa sare ya 2-2.
Habari Muhimu;
Chelsea; Eden Hazard atarudi kwenye majeruhi huku akiungana na kikosi mara baada ya kukosa mchezo mmoja kutokana na majeruhi, huku Chelsea ikimkosa mchezaji Ross Barkley ambaye alisajiliwa akiwa na majeruhi, ingawa maendeleo yake ni mazuri kwa sasa na alianza mazoezi pamoja na wenzake. Huenda akarudi katika mchezo wa Arsenal ambao Chelsea itakuwa ugenini au dhidi ya Norwich. Nje ya hapo hakuna majeruhi mwengine huku David Luiz na Charly Musonda wakiwa sawa.

Arsenal; Wao wanaweza kucheza bila huduma ya Aaron Ramsey na Olivier Giroud ambao wanatajwa kuwa majeruhi, lakini kuna taarifa zinaeleza kuwa kiungo wao Granit Xhaka naye ni majeruhi ingawa inawezakana mzee Arsene Wenger amesema ivi ili kuizubaisha Chelsea tu ambapo alifanya pia ivi katika mchezo uliopita dhidi ya Chelsea ambapo alisema Mesut Ozil ni majeruhi ila alikuwepo.
Mwamuzi; Martin Atkinson ndiye atakuwa mwamuzi katika mchezo huu wa leo ambaye alianza kuwa mwamuzi toka akiwa na miaka 16 ambapo kwa sasa ana miaka 46 akiwa ni mwamuzi aliye chini ya chama cha waamuzi wa soka Uingereza huku akiwa anatambuliwa pia na FIFA lakini atasaidiwa na refa wa video, Video Assistant Referee(VAR).
H2H; Katika michezo mitano iliyopita, Chelsea imeshinda 1 na kutoka sare michezo mitatu huku ikipoteza mchezo 1, ukihesabu sawa na ule mchezo wa kirafiki uliochezwa barani Asia.
Rekodi;
Chelsea: DWWDD
Arsenal; DWDDL
Chelsea: DWWDD
Arsenal; DWDDL
Muda; Saa 11:00 Usiku (Saa 23:00) kwa saa za Afrika Mashariki
No comments:
Post a Comment