LUKAZIGO ILIKUWA ATUE CHELSEA? - Darajani 1905

LUKAZIGO ILIKUWA ATUE CHELSEA?

Share This
Huenda hii ikawa ni habari ngumu kuiamini lakini mpia ikawa rahisi kuiamini, mmiliki wa klabu ya Everton amesema eti mshambuliaji wa sasa wa klabu ya MAnyumbu(Man utd), Romelu Lukaku au mashabiki wa Chelsea huwa tunapenda kumuita Lukazigo kutokana na uzito wake wa kushinda kunyumbulika na kutokuwa na kasi, eti ilikuwa atue Chelsea.

Lukazigo ambaye aliwai kuichezea Chelsea akisajiliwa akitokea klabu ya nchini Ubelgiji, Anderlecht, hiyo ilikuwa mwaka 2011 ambapo alikuja kuuzwa mwaka 2014 na kuuzwa kwenda Everton kabla ya dirisha kubwa la usajili lililopita kujiunga na Manyumbu kwa dau la paundi milioni 75 ilikuwa ajiunge tena na Chelsea ambayo ilitajwa kwa karibu kumsajili, kama anavyosimulia mmiliki huyo akisema "Nilitumia misimu mitatu kujaribu kumbakiza aendelee kuwa Everton, lakini alionekana akitamani kurudi Chelsea. Siku moja nikiwa nafanya nae mazungumzo alipokea simu kutoka kwa bibi yake aliyekuwa Afrika na hapo wakaongea kilugha na mwishowe bibi yake pia alimwambia ajiunge na Chelsea, lakini kama unavyojua nafasi ya mawakala katika miaka hii, wana nguvu kubwa katika kumshawishi mchezaji, mwisho nikaja kusikia alienda Los Angeles(ambako Manyumbu walienda kutumia muda wao wa mapumziko baada ya msimu kuisha), na ndio ikawa mwisho kuonana nae mahali hapa"

Mara baada ya Chelsea kumkosa Lukazigo ikamsajili Alvaro Morata kwa dau la paundi milioni 60

***je ulikuwa unatamani Lukazigo atue Chelsea? au mpaka sasa ukaambiwa nani bora kati ya Lukazigo na Alvaro Morata, je ungesema nani bora? unazani tumepatia kuachana nae au tulibugi?




No comments:

Post a Comment