CHELSEA YASHINDWANA NA ALEX SANDRO - Darajani 1905

CHELSEA YASHINDWANA NA ALEX SANDRO

Share This
Klabu ya Chelsea imekuwa ikitajwa kumfukuzia kwa karibu nyota wa klabu ya jijini Turin nchini Italia, Juventus anayecheza nafasi ya mlinzi wa kushoto, Alex Sandro lakini juhudi za Chelsea zinaonekana kugonga mwamba kila wanapopeleka ofa hiyo ili kumnasa nyota huyo.

Kuna ripoti imetoka kuwa klabu hiyo ya Juventus imetaja tena dau la nyota huyo ambapo klabu ya Chelsea itatakiwa kulitoa ili kumnasa nyota huyo ambaye kocha Antonio Conte anamtaka ili apate wachezaji wengi katika nafasi ya mabeki ambapo kwa upande wa Marcos Alonso kunaonekana kutopataikana mtu sahihi wa kumpa changamoto au ata kuwa mbadala pale ALonso anapopata majeruhi au inapobidi atolewe.

Paundi milioni 60 ndicho kiasi ambacho Juve wanakitaka ili kumuachia nyota huyo ingawa kwa Chelsea inaonekana kusita kutoa kisi hicho kwa mchezaji huyo ambapo imekuwaikimfukuzia toka dirisha kubwa la usajili lililopita kabla ya msimu huu kuanza.

No comments:

Post a Comment