CONTE AMWELEZEA HAZARD KUELEKEA CHELSEA vs ARSENAL - Darajani 1905

CONTE AMWELEZEA HAZARD KUELEKEA CHELSEA vs ARSENAL

Share This
Kuelekea mchezo wa leo usiku pale Darajani ambapo Chelsea itashuka uwanjani kumenyana na Arsenyani(Arsenal) katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la Carabao ambao ni mchezo wa kwanza huku kukiwa na mchezo wa pili ambapo Chelsea itacheza ugenini kwa hatua hiyohiyo ya nusu fainali, kocha Antonio Conte amemuelezea nyota wake Eden Hazard ambaye alilipotiwa kuwa na majeruhi na kukosa mchezo huo wa leo usiku.

Conte aliulizwa kuhusu kukaribia kwa winga wa Arsenyani, Alexis Sanchez kuondoka klabuni hapo katika dirisha hili la usajili je kunaweza kuchochea kwa nyota wake Hazard naye kuachana na klabu hiyo ambapo anatajwa kuhusishwa na tetesi za kuungana na Real Madrid "Siwezi kuongelea kilichotokea kwa wachezaji wa timu nyengine lakini kama mnavyojua Eden ni mchezaji wa muhimu sana kwetu na ana furaha kubaki hapa. Na tunataka kuwapatia furaha mashabiki wetu, lakini pia yupo sawa kucheza mchezo wa leo"

Hazard aliukosa mchezo wa kombe la FA mara baada ya kupata majeraha katika mchezo wa ligi kuu Uingereza aliposhuka uwanjani kumenyana dhidi ya Arsenyani wiki iliyopita ambapo mchezo huo uliisha kwa sare ya 2-2 huku Hazard akifunga kwa penati.

No comments:

Post a Comment