CONTE ALIMTAKA VAN DIJK - Darajani 1905

CONTE ALIMTAKA VAN DIJK

Share This
Kocha wa Chelsea amemzungumzia nyota mpya wa klabu ya Liverpunga(Liverpool) ambaye ni raia wa Uholanzi, Virgil Van Dijk ambaye alisajiliwa na klabu hiyo mapema katika dirisha hili dogo la usajili kwa dau la rekodi ya dunia ambapo usajili wake uliigharimu Liver kiasi cha paundi milioni 75 ambapo kwa dau hilo limemfanya kuwa mlinzi ghali zaidi duniani.

"Huu ndio mpira, huwezi kulaumu kwanini imekuwa ivi. Ila alikuwa chaguo letu, lakini kama unavyojua huu ndio mpira, na ndivyo ulivyo. Unaweza kuwa na nyota unaowataka ila usiwapate maana dirisha la usajili huwa ni gumu kwa kila timu" alisema Antonio Conte alipoulizwa juu ya nia yake ya kumtaka Van Dijk.

Chelsea ilikaribia kumpata nyota huyo katika dirisha kubwa lililopita mara baada ya kutokea mzozo kati ya klabu ya Southampton(klabu aliyotokea Van Dijk) na Liverpunga ambapo Southampton waliishtaki klabu ya Liver kutokana na kufanya mawasiliano na mlinzi wao bila kupata ruhusa kutoka kwa klabu yake kutokana na kuwa na mkataba bado na klabu hiyo, ila ushawishi wa Liver ulionekana kumwingia Van Dijk na kulazimisha uhamisho huo wa kutua kwa majogoo mpaka kufikia hatua kucheza soka la ovyo na hata kususia mazoezi ndipo Liver ikakamilisha usajili wake katika dirisha hili la usajili ambapo alisajiliwa kwa dau hilo.

No comments:

Post a Comment