ANDREAS AMWAGA WINO CHELSEA - Darajani 1905

ANDREAS AMWAGA WINO CHELSEA

Share This

Mlinzi wa kati raia wa Denmark anayeichezea klabu ya mabingwa Ulaya Chelsea, Andreas Christensen amesaini mkataba mpya klabuni hapo ambapo mkataba wake mpya ni wa miaka minne na nusu.

Christensen ambaye alitolewa kwa mkopo klabuni Borrusia Monchnglebach ya nchini Ujerumani ambapo huko alikaa miaka miwili kabla ya kurudi Chelsea ambapo toka amerudi mwanzoni mwa msimu huu amekuwa na kiwango bora akiliziba vyema pengo la beki mbrazili, David Luiz.

Amesaini mkataba huo leo akiwa anashuhudia na Marina Glanovskaia ambaye ni moja viongozi wa Chelsea.

No comments:

Post a Comment