Winga na mchezaji nyota wa Chelsea, Charly Musonda Jr huenda akajiunga na klabu yoyote ya nchini Uingereza kwa mkopo.
Winga huyo anaweza kujiunga na klabu itakayoonyesha nia ya kumtaka ili akacheze kwa mkopo mara baada ya kuonekana kupata nafasi katika kikosi cha Chelsea ni ngumu, ambapo kwa msimu huu amecheza mechi mbili tu za ligi kuu huku akiwa nje kutokana na majeruhi.
Musonda ambaye mapema kwenye msimu huu ametoka kusaini mkataba mpya wa kubaki Chelsea kwa miaka mingine mitano anataka kutolewa kwa mkopo kwenye ligi za Uingereza tu na sio nje ya hapo ili alizoee soka la nchini humo huku msimu uliopita alitolewa kwa mkopo Real Betis ya nchini Hispania kabla ya kuitwa tena na Chelsea mwezi januari mwaka jana.
No comments:
Post a Comment