CONTE AMUONGELEA BATSHUAYI - Darajani 1905

CONTE AMUONGELEA BATSHUAYI

Share This

Mara baada ya kuwepo tetesi kadhaa zikimhusisha mshambuliaji wa Chelsea, Michy Batshuayi ambaye ni raia wa Ubelgiji akitakiwa na baadhi ya klabu ikiwemo klabu kutoka nchini Hispania, Sevilla. Kocha wa Chelsea amejaribu kumuelezea nyota huyo anayeonekana kuwa na maisha magumu pale Chelsea kutokana na kutopewa nafasi hata pale anapokosekana Alvaro Morata ambaye ndiye mshambuliaji tegemezi basi huchezeshwa Eden Hazard katika nafasi hiyo na Batshuayi kuachwa benchi.

"Ni mchezaji mdogo na huwezi kumlaumu kushindwa kupata nafasi kwenye timu ya Chelsea, ila napenda kujituma na kupambana kwake. Kwa uchanga wake ni ngumu kuonyesha ubora kwa klabu kubwa kama Chelsea" alisema kocha Antonio Conte.

Batshuayi kwa sasa ana miaka 24 huku akicheza Chelsea kwa msimu wa pili sasa akitokea kwenye klabu ya Ufaransa inayoshiriki ligi kuu nchini humo maarufu kama Ligue 1, Olympique Marseille.

No comments:

Post a Comment