Mara baada ya kuwepo na tetesi za Chelsea ikimfukuzia nyota wa klabu ya Bayern Munich ambaye ni raia wa Chile, Artulo Vidal kabla ya tetesi hizo kugonga mwamba mara baada ya klabu ya Bayern kukataa kumuuza nyota huyo katika dirisha hili la usajili, sasa Chelsea inatajwa kwa karibu kumnasa kiungo raia wa Ubelgiji, Radja Nainngolan anayeonekana kuwa na maisha mafupi klabuni kwake kutokana na kuwa na maelewano mabovu na kocha wa timu hiyo.
Chelsea iliwai kumfukuzia nyota huyo kabla ya kiungo huyo mkabaji kusaini mkataba mpya klabuni As Roma inayotumia uwanja wa Stadio Olimpico uliopo nchini Italia.
Lakini sasa Chelsea inaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kumnasa kiungo huyo ambaye anatajwa kuwa na thamani ya paundi milioni 40 kutokana na maelewano mabovu aliyokuwa nayo na kocha wake.
Je Nainngolan atakubari kuungana na wabelgiji wenzake yaani Eden Hazard, Michy Batshuayi na Thibaut Courtois waliopo Chelsea?
No comments:
Post a Comment