BARKLEY KUWEPO CHELSEA vs ARSENAL? - Darajani 1905

BARKLEY KUWEPO CHELSEA vs ARSENAL?

Share This
Huenda unajiuliza kama nyota mpya wa Chelsea, Ross Barkley atakuwepo katika mchezo wa kesho dhidi ya Arsenyani(Arsenal) mara baada ya mchezaji huyo kuanza mazoezi akiwa klabuni Chelsea licha ya kutoka Everton akiwa majeruhi ambapo hajacheza kabisa msimu huu akiwa anauguza majeraha yake.

Sasa swali ni je, nyota huyo mwenye miaka 24 atacheza katika mchezo wa kombe la Carabao dhidi ya Arsenyani hapo kesho? jibu alilolitoa Conte ni Hapana, kutokana na mchezaji huyo kutokuwa sawa kwa asilimia mia moja kuweza kucheza mchezo huo.

"kesho usiku kucheza pamoja nasi, itakuwa ni mapema sana. Ingawa ameonyesha ukomavu katikamazoezi yake binafsi na hata ameshaungana na timu tayari akifanya mzoezi pamoja nasi, ila ni mapema sana maana inatakiwa awe sawa kama yeye lakini pia ajue tunacheza vipi kimfumo" alisema kocha Antonio Conte

Ross Barkley alikamilisha usajili wa kuungana na Chelsea siku ya ijumaa iliyopita akitokea klabuni Everton kwa dau la paundi milioni 15 huku akisaini kuichezea Chelsea mkataba wa miaka mitano na nusu ambapo inamaanisha mkataba wake utaisha mwaka 2023.

No comments:

Post a Comment