Chelsea katika dirisha hili la usajili imemsajili nyota Ross Barkley kutoka Everton ambaye yeye ataingia kwenye timu ya wakubwa, lakini pia ilimsajili kinda kutoka nchini Austria akiitwa Thierno Ballo ambaye yeye ataingia kwenye akademi ya Chelsea ambayo imekuwa na mwendelezo mzuri wa kutengeneza na kukuza vipaji.
Mpaka sasa akademi ya Chelsea imefanikiwa kuzalisha baadhi ya nyota ambao wengine wapo Chelsea ya wakubwa ambao ni kama Charly Musonda Jr, Andreas Christensen na hata Callum-Odoi ambaye yeye bado hajapata nafasi ya kuonekana zaidi lakini amekuwa na mfululioz mzuri akiwa Chelsea ya vijana. Lakini pia imekuwa na nyota iliywazalisha ambao kwa sasa wapo kwa mkopo klabu kadhaa kama Ruben Loftus-Cheek, Jeremie Boga, matt Miazga na hata Ola Aina na wengine wengi lakini pia kuna baadhi tayari washauzwa akiwemo Nathaniel Chalobah, Nathan Ake pamoja na Christian Atsu.
Sasa kuna ujumbe umetolewa na nyota wa zamani wa Chelsea, John Terry ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Aston Villa lakini huku akiwa katika mafunzo ya ukocha, ambapo ujumbe huo aliutoa haswa kuwalenga makinda na wanaosajiliwa na klabu hiyo ambao wameingia katika akademi "Naongea na wale wote waliokuja hapa kwenye akademi, usizani kuwepo kwako hapa ni kwa kuwa umekuja ili kuangalia baada ya miaka miwili utakuwa wapi na utakuwa kwenye mafanikio ya aina ganoi, umekuwa hapa utajifunza mengi kuhusu safari yako kisoka na hata elimu ya miasha, kwa upand wangu nilipokuwa hapa nilikuwa katika vikwazo na kufanikiwa nikiwa uwanjani na hata nje ya uwanja. Muhimu ni kupambana na kuwa na nia thabiti. Mara zote unatakiwa uwe mtu mwenye kuonekana unapambania mafanikio, hilo ndio jambo unalopaswa kulifanya"
John Terry akiwa Chelsea amefanikiwa kucheza kwa miaka 22 huku akiichezea klabu hiyo michezo 492 na kuifungia magoli 41.

JOHN TERRY AWAPA UJUMBE MAKINDA WA CHELSEA
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment