Kuelekea mchezo wa kesho jumatano ambapo Chelsea itaanzia nyumbani Stamford Bridge kucheza dhidi ya Arsenyani(Arsenal) katika mchezo wa hatua ya nusu fainali ya kombe la Carabao, mchambuzi wa soka maarufu Charlie Nicholas ambaye alishawai kuzichezea klabu za Celtic na Arsenyani ameipa ushindi Chelsea katika mchezo huo huku akiamini mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata ataiangamiza klabu hiyo.
"Haikuwa sawa ilipoisha 2-2 pale Emirates, Wenger(kocha wa Arsenyani) anatakiwa aiandae timu yake vyema na sio kile alichokitumia katika kombe la FA(alifungwa na kutolewa kwa mabao 4-2 dhidi ya Nottingham Forest). Sina matumaini makubwa kwa Arsenal, nadhani watapata bahati kwa kufunga goli moja tu. Lakini pia naweza kumuona Alvaro Morata akifanya makubwa, na huenda akafunga mara mbili ili kurekebisha makosa katika mchezo uliopita" alisema mchambuzi huyo ambaye enzi zake alicheza soka kama mshambuliaji.
Chelsea dhidi ya Arsenyani zilitoka kumenyana katika mchezo wa ligi kuu wiki iliyopita ambapo mchezo huo uliisha kwa sare ya 2-2 huku Alvaro Morata akionekana kukosa nafasi nyingi za wazi katika mchezo huo ambapo katika mchezo huo alikosa nafasi tatu ambazo angeweza kuipatia alama tatu muhimu kwa klabu yake.
Utabiri wake; Chelsea 3-1 Arsenyani
Je ataweza kurekebisha makosa?

MORATA ATAIANGAMIZA ARSENYANI
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment