CHELSEA YATAJIWA BEI YA MOURA - Darajani 1905

CHELSEA YATAJIWA BEI YA MOURA

Share This
Mara baada ya kuhusishwa na nyota wa klabu ya PSG, Lucas Moura sasa klabu ya Chelsea imetajiwa rasmi thamani na bei ya nyota huyo kama ikitaka kumsajili katika dirisha hili dogo la usajili ambapo mpaka sasa imeshafanikiwa kumnasa nyota mmoja kutoka Everton, Ross Barkley kwa dau a paundi milioni 15.

Katika kuhusishwa na nyota huyo kwa muda mrefu, sasa klabu ya PSG imesema kama kuna timu inamtaka nyota wao huyo ambaye ni raia wa Brazil basi italazimika kutoa kiasi cha paundi milioni 35 huku akihusishwa na vilabu kadhaa vinavyomhitaji huku mwenyewe akigoma kuendelea kubaki Ufaransa na anatazamia kutimkia Uingereza, je atatua Chelsea? na kumbuka Moura kwa sasa ana miaka 25 wakati Chelsea itaenda kuwapoteza au kutopata kile kiwango cha nyota kama Willian, Fabregas na Pedro kuokana na umri wao kuelekea uzeeni.

No comments:

Post a Comment