BARCA YAMPIGA CHINI LUIZ - Darajani 1905

BARCA YAMPIGA CHINI LUIZ

Share This

Huenda ikawa ni habari ngeni kwako, inawezekana vipi mchezaji apigwe chini na timu na sio timu ipigwe chini na mchezaji. Ila ndio ivo imetokea mara baada ya mlinzi wa Chelsea ambaye ni raia wa Brazil, David Luiz kupigwa chini na Barcelona.

Ilikuwa ivi, David Luiz alimwagiza wakala wake, Giuliano Bertolucci ili amtafutie klabu mpya mchezaji huyo apate nafasi ya kucheza zaidi ili amshawishi kocha wake wa Brazil, Tite aweze kumuita kwenye kikosi kitakachoenda kombe la dunia.

Ndipo wakala huyo akafanya mawasiliano na klabu ya Barcelona ili mchezaji wake ajiunge na klabu hiyo ya nchini Hispania. Lakini klabu hiyo imegoma kumsajili huku ikidai imetosheka na huduma ya walinzi wake wa sasa ambao inawatumia zaidi, Samuel Umtiti na Gerrard Pique.

Kwa maana hiyo beki huyo anatafuta pa kwenda kucheza ili aonekane na kocha wake huku akiona akiendelea kuwa Chelsea hatopata nafasi huku kocha Antonio Conte akitoa ruhusa kwa mchezaji yoyote atakayetaka kuondoka ili apate nafasi kwenye timu ya taifa kuwa anaweza kuondoka.

No comments:

Post a Comment