Mara baada ya kocha wa klabu ya Bayern Munich kukataa kumuuza mchezaji yoyote wa klabu huku akiigomea Chelsea kuwauzia Arturo Vidal ambaye alipendekezwa na kocha Antonio Conte ili asajiliwe klabuni Chelsea, sasa Chelsea imeachana na nyota huyo na sasa wanamtaka kiungo mwengine mwenye sifa za ubabe kama Vidal.
Radja Nainggolan wa klabu ya As Roma anatajwa kuingia tena kwenye rada za Chelsea ili asajiliwe kwenye dirisha hili dogo la usajili.
Nainngolan amekuwa akitakiwa na Chelsea mara kadhaa kabla ya kuikatisha tamaa Chelsea msimu uliopita mara baada ya kusaini mkataba mpya klabuni As Roma ingawa kwa sasa inatajwa kutokuwa na maelewano mazuri klabuni hapo akilalamikia kwa kuwa na tabia isiyopendeza.
Nainngolan inaelezwa aliachwa pia kwenye mchezo dhidi ya Atalanta ikielezwa sababu kubwa kutokana na utovu wake wa nidhamu.
Lakini kama Chelsea itapeleka ofa kwa mchezaji huyo imebainika itatakiwa iandae dau nono kutokana na nyota huyo raia wa Ubelgiji mwenye miaka 29 kutoka kusaini mkataba mpya mwaka jana. Ambapo kiasi kinachokadiriwa kumfanya aondoke ni paundi milioni 44.
No comments:
Post a Comment