Kumepangwa michezo ya raundi ya nne katika kombe la FA huku kukiwa na maswali mengi kuelekea raundi hiyo ya nne.
Lakini kubwa ni je Chelsea itacheza tena dhidi ya kocha wake wa zamani, Rafa Benitez? katika kombe hilo lenye heshima kubwa nchini Uingereza.
Lakini jibu hilo litajibiwa pale Stamford Bridge ambapo Chelsea itaikaribisha Norwich city kucheza mchezo wa hatua ya tatu wa kombe hilo ambapo katika mchezo wa kwanza uliisha kwa suluhu ya 0-0 katika uwanja wa Carrow Road ambapo kwa matokeo hayo ilimaanisha lazima warudiane. Ambapo baadae ikapangwa mchezo huo kuwa utachezwa tarehe 16-Januari. Na kama Chelsea ikishinda hapo basi itamenyana na Newcastle united iliyochini ya kocha Rafa Benitez katika raundi ya nne.
Katika mchezo wa kwanza ambapo kocha huyo aliiongoza Newcastle kucheza dhidi ya Chelsea ilikuwa katika ligi kuu, alipoteza kwa 3-1.
Na kama Chelsea na Newcastle zikikutana katika kombe hili la FA basi itamaanisha wataanzia Stamford Bridge.
No comments:
Post a Comment