RONALDO ATAMANI KUTUA CHELSEA - Darajani 1905

RONALDO ATAMANI KUTUA CHELSEA

Share This

Nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ambaye ni mshindi wa tunzo ya Ballon d'or yaani mchezaji bora wa dunia mara tano inaelezwa anatamani kujiunga na Chelsea ambayo inatajwa nayo kumtaka.

Taarifa kutoka gazeti moja nchini Uingereza linadai nyota huyo aliyeifungia Madrid magoli manne katika msimu huu wa ligi kuu Hispania maarufu kama La Liga amechagua kutua klabuni Chelsea huku akizani itakuwa ngumu kurudi Manyumbu {Man utd} alipotokea kabla ya kwenda Madrid kutokana na kutokuwa na mahusiano mazuri na kocha wa klabu hiyo, Jose Mourinho.

Ronaldo anataka kurudi Uingereza mara baada kuonekana kutopendezwa na mfumo wa nchini Hispania ambapo ndipo yupo huku swala la kulipa kodi ndilo linalotajwa kumchukiza.

Je unazani Chelsea inamhitaji Ronaldo? au aende sehemu nyengine?

No comments:

Post a Comment