Mara baada ya Chelsea kufanikiwa kumnasa nyota raia wa Uingereza, Ross Barkley kutoka klabuni Everton kwa dau la paundi milioni 15, nafasi yake uwanjani ndio imezua maswali kwa mashabiki wengi wa Chelsea.
Wengi wamekuwa wakijiuliza ni nafasi gani atakuwa anacheza kinda huyo mwenye miaka 24 kama akishapona na kuwa sawa kabisa? je atacheza kwa nafasi ya ushambuliaji au kiungo?
Kocha Antonio Conte amelijibu swali hilo ambapo amesema kama Chelsea itatumia mfumo wa viungo watatu katikati basi Barkley atacheza kama namba 10 ambapo atakuwa anacheza nyuma ya washambuliaji wawili wakati kama utatumika mfumo wa 3-4-3 basi atatumika kama mshambuliaji wa pembeni.
Lakini pia katika mkutano wa kocha huyo alipofanya na waandishi wa habari alisema Cesc Fabregas na Pedro wana miaka zaidi ya 30 huku pia Willian anatimiza miaka 30 mwaka huu kwa hiyo uwepo wa Barkley utaleta radha ya damu changa na kufanya apate muda mwingi wa kujifunza kutoka kwa waliomtangulia.
No comments:
Post a Comment