Kinachoendelea kwa sasa kinachomhusu kocha wa mabingwa watetezi, Chelsea, kocha Antonio Conte ni juu ya vita yake ya maneno na kocha wa zamani wa Chelsea ambaye kwa sasa ni kocha wa Manyumbu(Man utd), Jose Mourinho..
Lakini je wajua kuwa vita hiyo ya Conte na Mourinho ni ya muda mrefu? haijaanza leo.
Oktoba 2016 —Manyumbu(Man utd) yalifungwa 4-0 na Chelsea huku ukiwa mchezo wa kwanza Mourinho akirudi Chelsea kama kocha wa Manyumbu huku pia ukiwa mchezo wa kwanza kwa kocha huyo kucheza dhidi ya Chelsea huku mashabiki wa Chelsea wakitoa mabango yake ya kumsifia uwanjani na huku wakimuita Yuda Iskarioti yaani ni msaliti. Na kama utakuwa na kumbukumbu nzuri Antonio Conte alishangilia kwa bidii mpaka Mourinho alilalamika kuwa kocha huyo anamfanyia udhalilishaji.
Machi 2017 –Chelsea ya Antonio Conte ilikutana tena na Manyumbu ya Mourinho katika mchezo wa kombe la FA ambapo mchezaji wa Manyumbu alipewa kadi nyekundu uku Chelsea ikishinda 1-0, goli likifungwa na N'Golo Kante.
Julai 2017--Kocha Antonio Conte alipoulizwa atafanyaje kuelekea msimu mpya mara baada ya kuiongoza Chelsea kutwaa taji la ligi kuu, Conte alijibu kuwa atainusuru timu isianguke kama ilivyoanguka ikiwa chini ya Mourinho ambapo alipobeba kombe la ligi kuu mwaka 2015 akiwa Chelsea, msimu uliofata aliporomoka mpaka wakati anatimuliwa haikuwa hata katika nafasi sita za juu katika msimamo wa ligi kuu.
Oktoba 2017 –Ndipo ni kama vita ya maneno kwa makocha hawa ilipoanzia, mara baada ya kocha wa Manyumbu, Jose Mourinho kusema "Mimi sio kama hao makocha wengine wanaolialia kisa wachezaji wao kuwa majeruhi" huku Antonio Conte akimjibu kwa kusema "Aifatilie timu yake"
Novemba 2017 – Chelsea iliibamiza Manyumbu 1-0 pale Stamford Bridge huku goli hilo likifungwa na Alvaro Morata akipokea krosi murua kutoka kwa Cesar Azpilicueta. Lakini kwa makocha hao hawakushikana mikono baada ya mpira kuisha.
Januari 2018 – Sasa leo ndio kama vita yao imepambana moto, huku Mourinho ambaye anajulikana kwa kuwa na vita ya maneno na makocha wengi ndio kama imenoga kwa Conte, huku Conte ikionekana anampiga maneno makali kocha huyo mreno ambapo mwisho Mourinho ameitwa "Kajitu kadogo" na baadae Conte akasema yupo tayari wakutane sura kwa sura pale ambapo Chelsea itasafiri kuifata Manyumbu kwenye mchezo wa ligi kuu ambao utachezwa tarehe 25-Februari.
No comments:
Post a Comment