CONTE AINGIA VITANI TENA NA MOURINHO - Darajani 1905

CONTE AINGIA VITANI TENA NA MOURINHO

Share This

Mara baada ya kuwepo vita ya maneno kati ya kocha wa Chelsea, Antonio Conte dhidi ya kocha wa zamani wa Chelsea ambaye kwa sasa anaifundisha klabu ya Manyumbu(Man utd), Jose Mourinho, sasa vita hiyo imeamia pia kwenye usajili katika dirisha hili dogo la usajili.

Conte na Mourinho kwa kuziwakilisha klabu zao, zinamuwania nyota wa kiafrika anayotoka nchini Mali ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya nchini Ureno yaani FC Porto kwa nafasi ya ushambuliaji, Moussa Marega ambaye ana miaka 26.

Marega anawaniwa kwa karibu na Chelsea lakini huku Manyumbu na wao wakimlilia kwa karibu ambapo kuna taarifa zinadai ishapeleka dau ili kumng'oa mwafrika huyo.

Lakini Chelsea nayo haitaki kubaki nyuma katika hilo na imeonyesha nia na juhudi katika kuweka safu yake ya ushambuliaji iwe imara zaidi kwa kumuongeza Marega.

No comments:

Post a Comment