Mwaka 1876 kulianzishwa mpango wa ujengaji wa uwanja ambao mwak mmoja baaadae yaai mwaka 1877 uwanja huo ulikamilika na kufunguliwa ili kutumika ikiwa ni tarehe 28 mezi Aprili. Uwanja huo uliitwa Stamford Bridge au Stamfordesbregge ukimaanisha the "bridge at the sandy ford" ambao mpaka leo una uwezo wa kuingiza mashabiki 41,631 ukiwa na miaka 147, ambapo miaka 28 baadae ndipo ikaanzishwa klabu ya Chelsea na mtu mmoja aliyeitwa Gus Mears akipata ushirikiano kidogo kutoka kwa ndugu yake Joseph Mears kuianzisha klabu ambayo leo ni moja kati ya klabu kubwa barani Ulaya na duniani kwa ujumla.
Toka miaka hiyo ya 1905 ambapo ndio klabu hii ilipoanzishwa mpaka kufikia leo imetengeneza historia kubwa huku ikijivunia mafanikio maubwa ikiwa chini ya tajiri kutoka Urusi, Roman Abramovich.
Sasa eo katika ukurasa huu wa KTBFFH nataka nikujuze kuhusu sehemu ya uwanja wa Chelsea au jukwaa la uwanja huo ambao umekuwa ukifanyiwa marekebisho kuuweka sawa na kujaribu kuuweka katika hadhi ya kisasa mpaka kufikia leo. Sehemu hiyo ya uwanja inaitwa The Shed End.
Shed End ni jukwaa maarufu pale Stamford Bridge, ni jukwaa linalopatikana kusini mwa uwanja huo. Jina la Shed End lilipatikana kutoka kwa mashabiki ambapo kabla jukwaa hilo lilikuwa linaitwa Fulham Road End kutokana na uwanja huo kupatikana katika barabara au mtaa wa Fulham lakini mashabiki wakalibatiza jina hilo la Shed End mpaka klabu nayo ikalibariki jina hilo na kuamua kuliita jukwaa hilo jina hilo.
Yani kama wewe ni shabiki nguli na Chelsea damu yani husikii kitu unapoambiwa Chelsea basi jukwaa hili linakuhusu ambapo mashabiki wote wa Chelsea ambao wao ni kama wamekunywa maji ya bendera basi hupatikana katika jukwaa hili ambalo huchukua watu 6414.
Lakini pia mara kadhaa katika jukwaa hilo hukaliwa na mashabiki wa timu ya ugenini ambapo wana nafasi ya kupata tiketi 3000 tu kuweza kukaa katika jukwaa hilo. Wakati pia picha na makumbusho iliyo na picha za makongwe wa Chelsea inapatikana upande huu.
Lakini jambo ambalo huenda hulijui katika sehemu hii ya Shed End ni kuwa majivu ya gwiji wa Chelsea yaliwekwa pia upande huu wa Shed End, hiyo ilikuwa mwaka 2016.
Kama Mungu ainiwezesha ipo siku nitafika Stamford mimi kama Barnabas Gwakisa au Pacha wa Bakayoko na ni lazima nifike Shed End, Naomba Mungu anisaidie.
KTBFFH; FANYA TWENZETU SHED END
Share This
Tags
# Chelsea HD
Share This
About Darajani 1905
Chelsea HD
Labels:
Chelsea HD
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment