Goli la Giroud laibua kituko, unajua ni kituko gani? soma hapa - Darajani 1905

Goli la Giroud laibua kituko, unajua ni kituko gani? soma hapa

Share This

Huenda hukulishuhudia ili tukio maana lilitokea nyuma ya kamera, lilitokea kwenye mchezo uliopita wa Chelsea ambapo ilikuwa pale Wembley kucheza mchezo wake wa nusu fainali ya kombe la FA dhidi ya Southampton inayofundishwa na mchezaji wa zamani wa Chelsea, Mark Hughes. Ujue ni tukio gani? nipo hapa kukujuza.

Mara baada ya kipindi cha kwanza cha nusu fainali hiyo kuisha huku mchezo bado ukiwa na matokeo ya 0-0, mpira ulianza na zikatumika sekunde 30 tu kuifanya Chelsea ipate goli la kwanza toka kipindi cha pili kuanza. Goli lililofungwa na mshambuliaji raia wa Ufaransa, Olivier Giroud ambapo goli hilo ndilo lililoleta kioja au tukio hilo.

Wakati goli hilo linafungwa kuna wachezaji wa akiba wa Southampton bado walikuwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo. Wachezaji hao ni Manolo Gabbiadini, Nathan Redmond na Guido Carrillo ambapo ni Gabbiadini tu alilishuhudia goli hilo akiangalia kwenye televisheni ndogo lakini pia kwa upande wa Marcos Alonso wa Chelsea ambaye hakucheza mchezo huo kutokana na adhabu ya kufungiwa michezo mitatu kwenye mchezo huo alikuwa akiutazama kama shabiki, wakati goli hilo likifungwa naye hakulishuhudia, alikuwa pamoja na wafanyakazi na wapambe wa Chelsea.

Mara baada ya kulifunga goli hilo, mshambuliaji huyo alifanyiwa mabadiliko na nafasi yake ikichukuliwa na Alvaro Morata ambaye alifunga goli lililokamilisha ushindi wa mabao 2-0 na kuifanya Chelsea kutinga fainali ya kombe hilo ambapo itacheza dhidi ya Man utd mwezi ujao, mwezi May.

No comments:

Post a Comment