Mmiliki wa klabu ya Chelsea raia wa Urusi, Roman Abramovich anatajwa kutoa tamko kali kwa viongozi wa klabu hiyo juu ya mfumo na mwenendo wa usajili unaoendelea klabuni hapo.
Gazeti la Mirror limeripoti kuwa mmiliki huyo ametoa tamko kwa viongozi wa Chelsea kuwa waelekekeze nguvu kubwa kwenye usajili na hajali kama kocha Antonio Conte ataendelea kusalia klabuni hapo kwa msimu ujao au laah. Taarifa hiyo inasema kwamba Chelsea kutajwa kumfukuzia kwa karibu kiungo raia wa Ivory Coast anayeichezea klabu ya nchini Ufaransa, Jean-Michael Serri yote ni kutokana na mmiliki huyo kuagiza kuwa jambo kubwa kwa sasa ni kujipanga kusajili wachezaji wapya na ndio maana Chelsea imeshaweka mezani paundi milioni 30 ili kumnasa kiungo huyo.
Mmiliki huyo anatajwa kutofurahishwa kwa Chelsea kutajwa kuwafukuzia makocha mbalimbali ili kumrithi Antonio Conte na badala yake amesema kubwa ambalo viongozi hao wanatakiwa kulifanya ni kusajili wachezaji kwanza na kuhusu kocha hilo linaweza likakamilishwa baadae wakati tayari wachezaji washasajiliwa.
No comments:
Post a Comment