Klabu ya Chelsea imeonywa juu ya kutomtumia nyota wake Michy Batshuayi na badala yake kuwepo tetesi kuwa nyota huyo yupo njiani kuondoka klabuni hapo ambapo kuna taarifa zinamhusisha kutakiwa na klabu kadhaa ikiwemo klabu ya Sevilla ya nchini Hispania inayoshiriki ligi kuu nchini humo maarufu kama La Liga.
Mchambuzi wa soka wa chombo cha habari cha Sky Sports, Tony Gale ameitahadharisha Chelsea juu ya mchezaji huyo na kuwaambia waangalie wasije wakafanya makosa kama walivyofanya kwa nyota kadhaa wa zamani, Kevin De Bruyne na Mohammed Salah ambao nao hawakuwai kuaminika klabuni hapoo mpaka kufikia hatua kuuzwa kwa dau rahisi ingawa tena kwa sasa wamekuwa moto.
"Anapambana sana kwa sasa, anapambania kupata nafasi na Chelsea ni kama haifanyi chochote kwa ajili yake. Waangalie asije akawa kama kwa De Bruyne na Salah, walipouzwa kutokana na kutoonekana bora na baadae wakaja kuwika timu nyengine" alisema mchambuzi huyo aliyekuwa mlinzi wa West Ham.
Nyota huyo kwa msimu huu ameshaichezea Chelsea michezo 21 na amefunga magoli 9 huku akionekana kutokuwa kwenye mipango ya kocha huku mara nyingi akitumiwa Alvaro Morata.

CHELSEA YAPEWA ONYO KWA BATSHUAYI
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment