Leo katika viwanja vya Cobham stadium ambavyo vinatumiwa na Chelsea kufanyia mazoezi, kuliongezeka sura mbili mpya ambapo wachezaji, Olivier Giroud na Emerson Palmieri waliungana rasmi na nyota wenzao wa Chelsea katika mazoezi.
Walifanya mazoezi na klabu ili kujiandaa na mchezo wa jumatatu ijayo ambapo Chelsea itakuwa ugenini kupambana dhidi ya Watford na nyota hao wanaweza wakajumuika katika mchezo kwa kuwa wachezaji kamili wa Chelsea.
Olivier Giroud ametua Chelsea kwa dau la paundi milioni 18 huku akipewa mkataba wa mwaka mmoja na nusu wakati kwa Emerson amepewa mkataba wa miaka minne na nusu huku akisajiliwa kwa dau la paundi milioni 25 akitokea klabuni As Roma ya nchini Italia.
Nyota mwenzao wa Chelsea, N'Golo Kante ametoa neno akiwaelezea nyota hao wapya klabuni.
"Olivier Giroud namfahamu na ni mshambuliaji mzuri na anaweza akatusaidia kupata magoli zaidi na hata kutusaidia kushinda kitu msimu huu na hata baadae hivyohivyo kwa Emerson, naamini wote kwa pamoja wanaweza kuisaidia klabu kwa kushinda mataji, ingawa simfahamu vizuri Emerson ila nimepata taarifa kuwa ni mchezaji mzuri" alisema Kante.
Na alipoulizwa juu ya matokeo mabovu ya jana, Chelsea ikipoteza dhidi ya Afc Bournemouth ambapo ilifungwa 3-0.
"Bournemouth walicheza vizuri mchezo huo na ukiangalia walitushangaza kipindi cha pili maana kipindi cha kwanza tulitoka suluhu. Walitufunga magoli matatu ya haraka. Na ilikuwa ngumu kwetu kwenda nayo sawa ingawa tulitengeneza nafasi nyingi" alisema mchezaji huyo ambaye msimu uliopita aliisaidia vyema Chelsea kushinda taji la ligi kuu.
Je una maoni gani juu ya nyota hao wapya klabuni.
No comments:
Post a Comment