Mara baada ya kusajiliwa na Chelsea, nyota raia wa Ufaransa, Olivier Giroud amefanyiwa mahojiano na kuulizwa sababu haswa iliyomfanya kukubali kuachana na Arsenyani (Arsenal) na kutua klabuni Chelsea.
Nyota huyo alisajiliwa rasmi na kuwa mchezaji wa Chelsea jana huku akisaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu.
"Jambo muhimu zaidi lilikuwa ni kufanya mawasiliano na kocha Antonio Conte. Nilijiona kama nahitajika zaidi kwa jinsi alivyoongea nami na ni kama alihitaji zaidi kufanya kazi nami"
"Nami nilitaka kusaini Chelsea na si sehemu nyengine. Nilihitaji kupata nafasi ya kucheza zaidi. Nilihitaji pia kuendelea kucheza Uingereza na Chelsea lilikuwa chaguo sahihi kwangu maana pia ingenifanya niendelee kuwa ndani ya London"
"Lakini sababu kubwa na iliyonifanya niwe hapa ni ushindani zaidi, na hilo ndio limekuwa jambo langu la kwanza kulizingatia. Naamini kuwa kwangu hapa ni chaguo sahihi" alisema nyota huyo aliyesajiliwa kwa dau la paundi milioni 18.
Na alipoulizwa juu ya kocha Antonio Conte alisema "Simfahamu sana lakini napenda mfumo wake na jinsi anavyoyaendesha mambo yake akiwa uwanjani. Ana mfumo mzuri wa kufundisha soka na amekuwa imara zaidi haswa kwenye safu ya ushambuliaji ambayo imeundwa na nyota wazuri. Naamini nitafanikiwa zaidi nikiwa hapa"
Alipoulizwa juu ya viungo wa Chelsea, Tiemoue Bakayoko na N'golo Kante ambao kwa pamoja ni wafaransa kama yeye, alijibu "Nimewafamu hao tukiwa timu ya taifa, ni wachezaji wazuri na hodari na niliongea nao mara baada ya mchezo wa Arsenal dhidi ya Chelsea katika kombe la Carabao, na nilikuwa na furaha sana kuwaona. Nafamiana pia na Eden Hazard na David Luiz na nimecheza michezo mingi dhidi ya Azpilicueta. Wachezaji wengi hapa wanaweza kuongea kifaransa akiwemo pia na Thibaut (Courtois) na nadhani nitajumuika nao pamoja."
Giroud anaweza akatumika kwenye mchezo dhidi ya Watford utakaochezwa tarehe 5-Februari ambapo Chelsea itakuwa ugenini.
No comments:
Post a Comment