AKE AIOMBA RADHI CHELSEA - Darajani 1905

AKE AIOMBA RADHI CHELSEA

Share This
Aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Chelsea, Nathan Ake ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Afc Bournemouth na juzi aliiongoza vyema klabu yake kuifunga Chelsea magoli 3-0 huku mwenyewe akiwa mmoja wa wafungaji amerekebisha kile kilichokuwa kikifikiriwa haswa baada ya kupokea maneno mengi kutoka kwa watu wakimshangaa alipoifunga Chelsea na kushangilia ikionekana kama hakutoa heshima kwa klabu hiyo iliyomkuza.

Kupitia mtandao wa Twitter, nyota huyo alituma ujumbe na kusema amefurahishwa na ushindi waliopata kama klabu lakinim kushangilia kwake haikuonyesha kama haiheshimu klabu yake hiyo ila alikuwa akijipongeza kwa goli lake.

Nathan Ake ambaye ni raia wa Uholanzi amekuwa na kulelewa katika akademi ya Chelsea ambapo alitua hapo toka mwaka 2011 kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa mwaka 2012 na kucheza hapo mpaka mwaka 2017 alipouzwa rasmi kwenda Bournemouth kwa dau la paundi milioni 20.

No comments:

Post a Comment