PLY; CHELSEA YAJICHIMBIA KILELENI - Darajani 1905

PLY; CHELSEA YAJICHIMBIA KILELENI

Share This

Kikosi cha vijana wa akademi ya Chelsea maarufu kama Chelsea Youth chini ya miaka 18 wamepata ushindi muhimu dhidi ya watani wao wa jadi Fulham ambao nao wanapatikana magharibi mwa jiji la London.

Mchezo huo umeisha kwa ushindi mwembamba walioupata vijana hao wa Chelsea kwa goli 1-0, goli lililofungwa na nyota wa klabu hiyo, Charlie Brown (pichani) na kufanikiwa kufikisha magoli 14 kwa msimu huu katika mwendelezo wa ligi hiyo kwa vijana.

Kwa ushindi huo, unaifanya Chelsea U18 kujiweka vyema katika msimamo wa ligi kwa vijana wa umri huo kuendeleza pengo lake la alama sita huku wenyewe wakiwa kileleni mwa ligi hiyo. Huu ni ushindi wa saba mfululizo kwa hiyo.

No comments:

Post a Comment