PLW; MAN CITY vs CHELSEA, NANI NI NANI - Darajani 1905

PLW; MAN CITY vs CHELSEA, NANI NI NANI

Share This
Wakati Chelsea FC ikijandaa kusafiri mpaka kwenye jiji la Manchester huko nchini Uingereza kupambana dhidi ya Manyumbu (Man utd), dada zao au klabu ya soka ya wanawake, Chelsea Ladies wao tayari washatua kwenye jiji hilo kumenyana dhidi ya majirani wa Manyumbu, klabu ya Man city ambayo nayo ina timu kwa ajili ya soka la akina dada.

Chelsea itatua kwenye jiji hilo na kuanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo mgumu unaohusisha klabu zinazoshikilia nafasi ya kwanza na nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu kwa akina dada maarufu kama PLW.

Kama Chelsea ikifanikiwa kupata ushindi katika mchezo huo, basi itajiweka sawa katika msimamo wa ligi kuu na kujipa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo huku wakiwa wametoka kuibamiza klabu ya Yeovil kwa mabao 2-0 katika mchezo uliopita lakini pia ikijihakikishia vyema kucheza hatua inayofata ya kombe la FA kwa wanawake ambako huko wamepangwa kumenyana dhidi ya Liverpumba (Liverpool).

No comments:

Post a Comment