ANTONIO CONTE ATOA MAJIBU KUELEKEA MCHEZO DHIDI YA MAN UTD - Darajani 1905

ANTONIO CONTE ATOA MAJIBU KUELEKEA MCHEZO DHIDI YA MAN UTD

Share This
Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amekuwa akihusishwa juu ya kuondoka klabuni hapo na kutimkia nchini Italia huku pia kukiwa na fununu za kocha huyo kutakiwa na vilabu kama PSG ya nchini Ufaransa pamoja na Real Madrid ya nchini Hispania. Kocha huyo amekuwa akihojiwa juu ya hali yake ya kuendelea kubaki klabuni Chelsea, huku waandishi wengi wa habari wakimtaja kuondoka klabuni hapo kutokana na mfumo wa usajili ulivyo huku akikaririwa mara kadhaa kuwa hapati nafasi kubwa ya kufanya usajili klabuni hapo ambapo kauli hiyo ilikaririwa kwamba hana muda mrefu klabuni hapo.

Kocha huyo amejibu tuhuma hizo huku akikadhia kuwa ana furaha ya kuendelea kubaki Chelsea na hana nia ya kuondoka klabuni hapo "Ni mchezo mmoja tu nilioshuhudia tukikosa hali ya mchezo na kukosa maarifa ya kuukabili, mchezo dhidi ya Watford (Chelsea ilipoteza kwa 4-1) hatukua sawa. Toka mwanzoni mwa msimu kwa kila mchezo tumekuwa sawa na tumekuwa na nidhamu ya hali ya juu"

"Kumekuwa na maelewano makubwa na kucheza kitimu katika kila mchezo. Lakini nimeshaliongea hili sana, nina furaha ya kuwa kocha kwa wachezaji wangu. Nina uhakika wa 100% wa kuendelea kuwa kocha wa wachezaji hawa, na ninafuraha kuwa hapa"

"Fikra za kupata ushindi zinakuja pale unapokuwa na maandalizi mazuri katika kujiandaa kwako na mchezp, na ubora wako na kupambana kwako ukiwa mazoezini, muda wote inabidi uwe kamili na mahusiano mazuri na kuelewana na kocha wako, wachezaji wenzako, mashabiki na wachezaji wa timu pinzani. Hapo ndipo fikra ya ushindi inapokuja na kuanzia" alisema kocha huyo.

Chelsea inajiandaa kucheza mchezo wake wa muhimu hapo kesho katika raundi ya 28 ya ligi kuu nchini Uingereza maarufu kama Premier League dhidi ya Manyumbu (Man utd), mchezo utakaochezwa kesho jumapili, na utamu wa mchezo huu unaletwa na nafasi za klabu hizo kwenye msimamo wa ligi kuu ambapo Chelsea inashika nafasi ya nne, huku ikiwa imezidiwa alama tatu na wapinzani wao hao wakati pia mchezo huo unanogeshwa na kumbukumbu ya vita ya maneno iliyokuwepo kati ya kocha Antonio Conte dhidi ya kocha wa Manyumbu, Jose Mourinho ambaye mwenyewe aliwai kuwa kocha wa Chelsea kabla ya Conte kutua klabuni hapo.

No comments:

Post a Comment