CHELSEA YAMTAMANI TENA HAZARD - Darajani 1905

CHELSEA YAMTAMANI TENA HAZARD

Share This
Klabu ya Chelsea ilianza kuonyesha nia ya kumtaka tena nyota wake wa zamani, Thorgan Hazard ambaye hakufanikiwa kuichezea mchezo wowte klabu ya Chelsea mpaka alipotolewa kwa mkopo kwenye klabu ya Zulte waregem na baadae Borrusia Monchengladbach ambapo huko ndio anapocheza mpaka sasa akiwa ameuzwa kwa uhamisho wa jumla.

Chelsea ilianza kuhusishwa tena kumtaka winga huyo ambaye ni mdogo wa nyota wa Chelsea, Eden Hazard katika dirisha dogo la usajili la mwezi wa kwanza lakini ikaeleweka kuwa ngivu wanayotaka kutumia ili kumnasa nyota huyo sio katika kipindi cha dirisha hilo, ila mpaka mwisho wa msimu katika dirisha kubwa la usajili.

Chelsea inataka kumrudisha kinda huyo ambaye aliwai kusajiliwa hapo kabla na Chelsea mwaka 2012 na mpaka sasa ameshaichezea klabu yake hiyo ya Borrusia Monchengladbach michezo 26 na kuifungia magoli nane huku akitengeneza mengine nane anatajwa kuwa na thamani ya paundi milioni 28 (Tanzania sh. 88 bilioni) huku akiwa na miaka 24 kwa sasa.

No comments:

Post a Comment