COURTOIS KUONDOKA CHELSEA? SABABU NI HIZI - Darajani 1905

COURTOIS KUONDOKA CHELSEA? SABABU NI HIZI

Share This
Klabu ya Chelsea inatajwa kuelekea kumpoteza mlinda mlango wake nambari moja, Thibaut Courtois ambaye kwa sasa ana miaka 25 mara baada ya kuhusishwa kwake kutakiwa kwa karibu na klabu ya nchini Hispania, Real madrid, ambao wanataka kumsaka mlinda mlango atakayeweza kutumika kama mlinda mlango nambari moja klabuni hapo, huku usajili huo ukichangizwa na mambo matatu.

Jambo la kwanza ni familia ya nyota huyo, ambao ni mke wake na watoto wake wawili ambao wanaishi nchini Hispania kwenye jiji la Madrid, jiji ambalo inatokea klabu hiyo. Thibaut Courtois wakati akiwa kwa mkopo kwenye klabu ya Atletico Madrid, alipata familia akiwa kwenye jiji hilo na mpaka leo bado wanaishi huko ambapo hiyo inatajwa kuwa sababu kubwa kwa nyota huyo kujiunga na klabu hiyo ili aweze kuungana tena na familia yake. Na mara kadhaa amewai kusikika akisema ingawa ana furaha kucheza Chelsea, ila moyo wake upo kwenye jiji hilo la Madrid ambapo ndipo familia yake inapoishi.

Jambo la pili ni uhakika wa kupata nafasi kwenye kikosi cha Madrid, bila shaka hakuna la kupinga kuwa nyota huyo endapo akitua Real Madrid basi matakuwa na nafasi ya uhakika kwenye kikosi cha kwanza, haswa ukizingatia kipa aliyepo kwa sasa, Keylor Navas kuonekana hana muda mrefu klabuni hapo na anaonekana hana muda mrefu wa kuendelea kubaki klabuni hapo.

Jambo la tatu na la mwisho, kumekuwa na taarifa zinazoaminika kuwa ni za kweli kwamba mlinda mlango, David de Gea anafanya mazungumzo na klabu yake ili asaini mataba mpya na klabu yake hiyo ambapo kwa taarifa hizo zinamaanisha kuwa Real Madrid hawatokuwa na chaguo jengine zaidi za kumchukua Thibaut Courtois. Mlinda mlango aliyekuwa akitajwa kutakiwa kwa karibu na klabu ya eal Madrid, ni David de Gea ambaye ni mlinda mlangowa klabu ya manyumbu (Man utd) lakini kusaini mkataba mpya itamaanisha kuwa inabidi litumike chaguo la pili ambaye ni Courtois.

Kocha Antonio Conte aliwai kuulizwa juu ya nini anakiona juu ya Thibaut Courtois pamoja na Eden Hazard ambao wote wanatajwa kutakiwa na Real Madrid, kovha huyo alisema unapowauza wachezaji kama Eden Hazard pamoja na Thibaut Courtois inakubidi utambue hakuna kiasi chochote utakachokitoa kuwapata wachezaji wengine waliokuwa bora kama hao, inatakiwa wabaki na waendelee kuwa Chelsea. Nasi kama mashabiki tunaungana na maneno ya Conte tukisema hatuhitaji nyota huyu pamoja na Hazard au hata mwengine yoyote bora kikosini akaondoka kwa njia yoyote.

No comments:

Post a Comment