Cesc Fabregas amchana Morata atoa sifa kibao kwa Giroud - Darajani 1905

Cesc Fabregas amchana Morata atoa sifa kibao kwa Giroud

Share This

Chelsea inacheza mchezo wake wa raundi ya 37 kwa ligi kuu Uingereza usiku huu dhidi ya Huddersfield kwenye uwanja wa Stamford Bridge, mchezo ambao Chelsea inahitaji iondoke na ushindi wowote ili iweze kuvuna alama tatu zitakazochochea mbio zake za kupambania nafasi ya klabu nne za juu kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza ili ifanikiwe kufudhu kucheza michuano ya klabu bingwa barani Ulaya maarufu kama UEFA Champions League.

Lakini nyota wa Chelsea, Cesc Fabregas ambaye mwanzoni mwa mwezi huu, mwezi May alitimiza miaka 31 amefanyiwa mahojiano na kueleza sababu haswa iliyoifanya klabu yake kuwa na wakati mgumu wa kupambania nafasi ya kucheza michuano hiyo ya Ulaya kwa msimu ujao ambapo ili ifanikiwe kucheza michuano hiyo basi italazimika ishinde michezo yote ya ligi iliyosalia (michezo 2) lakini ikitegemea matokeo ya Tottenham na Liverpool.

" Tunapata nafasi nyingi maana timu yetu ni timu inayostahili ushindi, na hilo ndio jambo muhimu. Nafikiri hilo ni pamoja na nafasi ya ulinzi nayo pia"

"Lakini lawama zetu na tutajilaumu haswa kutokana na safu yetu ya ushambuliaji, maana imekua haitumii vilivyo nafasi tunazozitengeneza. Tumekuwa tukitengeneza nafasi nyingi nyingi sana za kufunga ambazo kama tungezitumia vyema basi tungeshinda michezo mingi haswa ile tuliyoshindwa kuondoka na ushindi. Tungeweza kushinda michezo mingi kama tungecheza kwa umakini na tahadhari kubwa, naamini huo ndio uliokua udhaifu wetu kwa msimu mzima"

Nyota huyo alipoulizwa kuhusu uwepo wa Olivier Giroud tangu asajiliwe klabuni hapo, Cesc alijibu akisema "Olivier anatusaidia sana haswa kwenye nafasi tulizokua tunapata tabu. Jambo muhimu ni kwamba anafunga magoli muhimu ambayo tunayahitaji haswa kwa mtu kama mimi ninayecheza kama kiungo, hivi ndivyo tunavyotaka, mshambuliaji kuzitumia nafasi anazozipata na kuifanya timu iondoke na ushindi" alisema nyota huyo akitoa sifa kwa mshambuliaji raia wa Ufaransa ambaye alisajiliwa na Chelsea kwenye dirisha dogo la usajili la mwezi Januari.

Alvaro Morata ambaye amekuwa akitumika kama mshambuliaji chaguo la kwanza kwenye kikosi cha Chelsea cha msimu huu na mpaka sasa ameshaichezea michezo 45 na ameifungia magoli 15.

No comments:

Post a Comment