Habari muhimu kuelekea Chelsea vs Huddersfield - Darajani 1905

Habari muhimu kuelekea Chelsea vs Huddersfield

Share This

Mapambano yanaendelea, mara baada ya Chelsea kuondoka na ushindi muhimu kwenye mchezo uliopita dhidi ya Liverpool, ushindi unaofufua matumaini mapya kwa klabu hiyo kushiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya kwa msimu ujao pale itakapofanikiwa kuingia kwenye klabu nne za juu kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza.

Hapa nakuletea habari muhimu kuhusu mchezo wa leo ambapo Chelsea inashuka uwanjani kucheza mchezo mwengine wa ligi kuu Uingereza dhidi ya Huddersfield ambao unakua mchezo wa raundi ya 37 ya msimu wa 2017-2018.

Habari muhimu;
Chelsea; Alvaro Morata anarejea uwanjani akitoka kwenye majeraha ya muda mfupi yaliyomfanya kuukosa mchezo uliopita dhidi ya Liverpool ambapo kocha Antonio Conte alisema nyota huyo hana majeraha yatakayomweka nje muda mrefu na hatimaye jana kwenye mkutano alioufanya na waandishi wa habari akakiri akisema nyota huyo yupo tayari kurejea uwanjani.

Kuhusu wachezaji walio na majeraha ni walewale walinzi wawili ambao ni David Luiz na Ethan Ampadu ambao bado wataendelea kuuguza majeraha yao.

Huddersfield; Tom Ince anarejea kwenye mchezo huu mara baada ya kuwa majeruhi wakati Tarence Kongolo na Chris Löwe wote wana hatihati ya kucheza kwenye mchezo huu kutokana na walipopata majeraha kwenye mchezo uliopita dhidi ya Manchester city

Mwamuzi; Lee Mason, atakuwa mwamuzi kwenye mchezo wa leo ambapo kwa msimu huu ameshakua mwamuzi dhidi ya Chelsea katika michezo minne huku akikumbukwa pia kwenye mchezo dhidi ya Swansea ambapo kocha Antonio Conte alipewa adhabu na mwamuzi huyo.

Rekodi;
➡Mara ya mwisho kwa Chelsea kucheza dhidi ya Huddersfield kwenye uwanja wa Stamford Bridge ilikuwa mwezi Februari mwaka 1984 ambapo ilipokea kichapo cha mabao 3-1.
➡Chelsea imeshinda michezo tisa katika michuano yote dhidi ya timu zilizochini ya majiji (Towns) kama ilivyo kwa Huddersfield Town ambapo imefanikiwa kuzibamiza magoli 32 huku ikiruhusu kufungwa magoli 6.
➡Huddersfield imeshindwa kufunga goli lolote katika michezo 20 kati ya 36 ya ligi kuu kwa msimu huu, ni timu mbili tu zimeizidi klabu hiyo kwenye rekodi mbovu ambazo ni Derby County (michezo 22 kwa msimu wa 2007-2008) na Leeds United (michezo 21 kwa mwaka 1996-1997)
➡Huddersfield imetoa suluhu katika michezo 13 ya ligi kuu ikiwa ugenini kwa msomu huu ambapo hiyo ni sawa na Norwich ambao walifanya hivyo kwa msimu wa 1994-1995 na Middlesbrough kwa msimu wa 2002-2003.

Michezo iliyopita;
Chelsea: DWWWW
Huddersfield: LDWLD

Muda; Saa 09: 45 Usiku (Saa 21:45) kwa saa za Afrika Mashariki (EAT)

No comments:

Post a Comment