Kikosi cha vijana cha Chelsea ambacho kinajulikana kama Chelsea Development kimecheza mchezo wake wa ligi kuu Uingereza 2 (Premier League 2) usiku wa leo dhidi ya Liverpool kwenye uwanja wa Anfield ambapo imepoteza kwa magoli 5-1 ikiwa ugenini.
Kikosi hicho kinachoundwa na wachezaji makinda zaidi kimepoteza mchezo huo wa ligi kuu na kuifanya kumaliza katika nafasi ya nane katika msimamo wa ligi hiyo ambapo sababu ya kufanya vibaya ni kutokana na mjumuisho wake wa wachezaji makinda zaidi tofauti na klabu nyengine kwenye.
Mchezo huo ni wa mwisho kwa kikosi hicho kwa msimu huu ambapo imefanikiwa pia kufikia hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la Checkatrade pamoja na kufanya vizuri kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa vijana.
No comments:
Post a Comment