Newcastle wapanga kuanza mazungumzo ya kumnasa Kenedy - Darajani 1905

Newcastle wapanga kuanza mazungumzo ya kumnasa Kenedy

Share This

Klabu ya Newcastle united ya nchini Uingereza inajiandaa kufanya mazungumzo na klabu ya Chelsea ili iweze kumsajili winga wa klabu hiyo aliyepo Newcastle united kwa mkopo,  Robert Kenedy ambaye ana uwezo pia wa kucheza kama mlinzi wa kushoto.

Nyota huyo raia wa Brazil alijiunga na Newcastle united kwa mkopo kwenye dirisha dogo la usajili la mwezi Januari na tangu atue klabuni hapo amekua akionyesha kiwango na uwezo wa hali ya juu hali iliyomfanya kocha wa klabu hiyo Rafa Benitez ambaye aliwai pia kuifundisha Chelsea kukiri kuwa anamuhusudu nyota huyo na atauagiza uongozi wa klabu yake ufanye mazungumzo na klabu ya Chelsea ili iweze kumnasa winga huyo.

Kenedy alitua Chelsea akitokea klabu ya Fluminense ya nchini Brazil haonekani kuhitajika tena kwenye kikosi cha Chelsea haswa kutokana na nafasi yake kutumiwa na nyota Marcos Alonso ambaye mbadala wake ni Emerson Palmieri hali inayoonyesha ufinyu wa winga huyo kupata nafasi kwenye kikosi hicho cha Chelsea.

No comments:

Post a Comment