Kocha wa klabu ya Leicester city, Claude Puel amehuzunishwa na taarifa za nyota wa klabu yake Riyad Mahrez kuhusishwa kutakiwa na klabu ya Chelsea na klabu nyengine ambazo zimekuwa zikitajwa kumuwania.
"Ni taarifa mbaya kwangu na kwa klabu, nampenda Riyad(Mahrez) amekuwa nyota wa timu na akicheza vizuri sana, nadhani itakuwa taarifa mbaya kwangu na kwa timu kama akiachana nasi" alisema Puel ambaye amechukua majukumu ya kuinoa klabu hiyo msimu huu
Mahrez amekuwa akitajwa kuhusishwa kuondoka klabuni hapo toka katika dirisha la usajili lililopita huku akikaribia kusajiliwa na AS Roma ambayo ilikuwa tayari kutoa paundi milioni 27 ambayo baadae ilikataliwa na Leicester.
Chelsea ipo tayari kumsajili nyota huyo ambaye mkataba wake na Leicester city unaisha mwaka 2020.
Je unazani Chelsea inamhitaji nyota huyo?
No comments:
Post a Comment