Mchezaji wa Bayern Munich, Artulo Vidal ambaye ni raia wa Chile anatajwa kutakiwa na klabu ya Chelsea ambapo kumekuwa na taarifa kuwa kocha Antonio Conte amefanya nae mawasiliano na nyota huyo ili aungane nae tena klabuni Chelsea.
Antonio Conte alishawai kumfundisha Vidal pindi alipokuwa klabuni Juventus kabla ya nyota huyo kuungana na Bayern.
Chelsea inamtaka kiungo huyo raia wa Chile ili aungane na klabu hiyo ya London ambapo kocha Conte anataka kuifanya klabu hiyo iwe na kikosi kipana kuelekea mzunguko wa pili ambao huwa ni mgumu.
No comments:
Post a Comment