Kocha wa Chelsea, Antonio Conte anatajwa kumuwania mlinzi wa Juventus ambaye ni raia wa Italia, Giorgio Chiellini ambaye alishawai kuwa chini ya kocha huyo pindi alipokuwa klabuni Juventus na hata timu ya taifa ya Italia.
Lakini kuna kikwazo kwa nyota huyo ambapo kuna taarifa zinadai kuwa nyota huyo hataki kuondoka klabuni hapo, na anapaona hapo ni kama nyumbani.
"Hapana sitaki kuondoka klabuni hapa, kwangu ni kama familia. Nasubiri kipindi iki cha sikukuu kipite ili nifanye mawasiliano na klabu ili nisaini mkataba mpya" alikaririwa Chiellini.
Conte anamtaka pia mlinzi wa AC Milan, Leonardo Bonucci ambaye naye alishakuwa chini ya kocha huyo Antonio Conte pindi alipokuwa klabuni Juventus na timu ya taifa ya Italia.
No comments:
Post a Comment