Kocha wa Arsenyani(Arsenal), Arsene Wenger leo amefanya mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kesho wa ligi kuu Uingereza, dhidi ya Chelsea.
Na katika mkutano huo, Wenger aliulizwa kuhusu kumtaka mlinzi wa Chelsea, David Luiz na kocha huyo kudai hizo taarifa sio za kweli.
"Hakuna ukweli kwenye taarifa hizo" alijibu Arsene Wenger.
David Luiz anaonekana kupoteza nafasi yake katika kikosi cha kwanza cha Chelsea, huku kinda Andreas Christensen akionekana kutumika zaidi ambapo mchezo wa mwisho kwa Luiz kuichezea Chelsea ilikuwa mwezi Oktoba mwaka 2017 mara baada ya mchezo wa klabu ya mabingwa Ulaya dhidi ya AS Roma ambapo Chelsea ilifungwa 3-0.
No comments:
Post a Comment