OSCAR RASMI UCHINANI - Darajani 1905

OSCAR RASMI UCHINANI

Share This

Tarehe kama ya leo mwaka 2017, yaani mwaka mmoja umetimia toka aliyekuwa kiungo mahiri wa Chelsea, Oscar Emboaba Junior aungane rasmi na klabu ya Shanghai SIPG akitokea Chelsea.

Chelsea ilimnasa kiungo huyo aliyezaliwa mwezi Septemba mwaka 1991 kwa dau la paundi milioni 19 akitokea Internacional mwaka 2012 akipishana na mkongwe Didier Drogba na badala yake akachukua namba ya mgongoni ya mkongwe huyo, akivaa namba 11.

Mwaka jana yaani 2017 tarehe kama ya leo nyota huyo alijiunga rasmi na klabu ya China ya Shanghai SIPG kwa dau la paundi milioni 52. Ambapo aliichezea Chelsea michezo 131 na kuifungia magoli 21.

Mpaka anaondoka Chelsea aliisaidia kutwaa mataji kadhaa lakini yakiwemo ya ligi kuu Uingereza mara mbili, Uefa Ueropa League mara moja na kombe la ligi mara moja.

Unakumbuka nini kutoka kwa Oscar? Mi nakumbuka ule mchezo wake wa kwanza baada ya kusajiliwa alipocheza dhidi ya Juventus akifunga magoli mawili huku Gigi Buffon, akitoa sifa nyingi kwa Oscar, na kama una kumbukumbu vizuri kocha wa Juventus kipindi icho alikuwa ni Antonio Conte, na toka mchezo ule, Conte alimfukuzia sana kwenye usajili ili amsajili atue Juventus kabla ya kuja kukutana nae Chelsea na kumkuta Oscar hayupo kwenye hali nzuri kisoka.

No comments:

Post a Comment