OZIL KUIKOSA CHELSEA - Darajani 1905

OZIL KUIKOSA CHELSEA

Share This

Kiungo raia wa Ujerumani, Mesut Ozil anatajwa kuukosa mchezo wa jumatano ambapo klabu yake ya Arsenyani(Arsenal) itashuka uwanjani kuikaribisha Chelsea katika mchezo wa ligi kuu Uingereza.

Inaelezwa kuwa Ozil ataukosa mchezo huo utakaochezwa siku ya tarehe 03-Januari ambapo Chelsea itashuka katika mchezo huo ikiendelea kuwakosa David Luiz na Charly Musonda wanaotegemewa kuwa sawa katika mchezo dhidi ya Norwich siku ya tarehe 06-Januari katika kombe la FA.

Kocha Arsene Wenger wa Arsenyani alipohojiwa kuhusu uwezekano wa mjerumani huyo katika mchezo wa raundi ya 22, alisema ana majeruhi na hivyo huenda akampumzisha katika mchezo huo.

Lakini hii sio mara ya kwanza kwa Wenger kusingizia mchezaji wake ni majeruhi maana alishawai kusema hivyo alipomenyana na Manyumbu(Man utd) akidai Alexzander Lacazette ni majeruhi na kumbe aliongopa.

Lakini pia Arsenyani itaendelea kumkosa mshambuliaji Olivier Giroud katika mchezo huo ambaye nae anashambuliwa na majeruhi.

No comments:

Post a Comment