CONTE AANZA MWAKA 2018 KUPAMBANA NA MAN CITY - Darajani 1905

CONTE AANZA MWAKA 2018 KUPAMBANA NA MAN CITY

Share This

Chelsea imemaliza mwaka 2017 ikipanda kutoka nafasi ya tatu mpaka nafasi ya pili ikifanikiwa kuishusha Manyumbu (Man utd) iliyokuwa kwenye nafasi hiyo, na sasa Chelsea ina alama 45 huku klabu ya Mama site(Man city) ikiwa kileleni kwa alama 59, ikiiacha Chelsea alama 14.

Mara baada ya kuingia mwaka 2018 ambao ndio utakuwa mwaka wa mwisho katika kukamilisha mzunguko wa pili wa msimu wa 2017/2018, kocha Antonio Conte ni kama amezinduka na kusema "Sasa mapambano dhidi ya Manchester city ndio yameanza rasmi"

Kocha huyo alipohojiwa alisema "Naiheshimu sana Mama site(Man city) lakini sasa nataka kupambana naye katika ligi kuu, iwe msimu huu au ata msimu ujao, lakini ni lazima tupambane nayo"

Chelsea ndiye bingwa mtetezi wa taji la ligi kuu ililobeba msimu uliopita na sasa imefanya makubwa msimu huu licha ya kutopewa nafasi na watu wengi wakiwemo wachambuzi wa soka huku wengine wakimtabiria mabaya kocha huyo muitaliano.

No comments:

Post a Comment