Kuna uwepo wa taarifa kwamba kocha Thomas Tuchel amekuwa akiitaka bodi ya Chelsea kufanya haraka kumpa mkataba mpya nyota Antonio Rudiger ili aendelee kusalia klabuni hapo.
Taarifa zinasema Chelsea na Rudiger wameshindwa kufikia makubaliano ya kusaini mkataba mpya kutokana na mshahara ambapo ofa ya Chelsea ya mshahara wa paundi 125,000 (Tsh. milioni 392) kwa wiki kuonekana kutomvutia nyota huyo.
Nyota huyo alipoulizwa kuhusu mustakabali wake wa kuendelea kusalia Chelsea amesema hilo ndilo jambo lililo akilini mwake kwamba anataka kuendelea kubaki klabuni hapo.
No comments:
Post a Comment