CONTE ATAMANI MAKUBWA KUTOKA KWA DRINKWATER - Darajani 1905

CONTE ATAMANI MAKUBWA KUTOKA KWA DRINKWATER

Share This

Nyota mpya wa Chelsea, Danny Drinkwater ambaye 'weekend' iliyopita aliiongoza Chelsea kuibamiza magoli 5-0 dhidi ya Stoke city ambaye nae aliifungia Chelsea goli lake la kwanza toka aungane na klabu hiyo anategemewa kufanya makubwa klabuni hapo.

Kocha Antonio Conte kuelekea mchezo dhidi ya Arsenal kesho amesema "Nategemea makubwa kutoka kwake, aliposajiliwa alikuwa na majeruhi kwa hiyo ilimchukua muda kidogo kuweza kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza kutokana na majeruhi yake"

"Nalifahamu alipokuwa Leicester alikuwa anacheza sambamba na Kante na naona akiwa hapa atapata nafasi zaidi akiwa pamoja nae"

"Nategemea kupata mambo makubwa kutoka kwake" alisema Conte.

Chelsea kesho itashuka uwanjani kumenyana na Arsenal katika mchezo wa ligi kuu Uingereza raundi ya 22 ambapo Chelsea itahitaji kupata ushindi katika mchezo huo ili kuweza kurudi kwenye nafasi yake ya pili ambapo jana imeshushwa jana mara baada ya Manyumbu(Man utd) kushinda mchezo wake dhidi ya Everton.

No comments:

Post a Comment