CHELSEA ITAIPA TABU MAN CITY - Darajani 1905

CHELSEA ITAIPA TABU MAN CITY

Share This

Mchambuzi wa soka maarufu kama Pat Nevin anadhani kama ingetokea Chelsea ingeachwa kwa alama chache na Mama site(Man city) basi leo, Chelsea ingeukaribia ubingwa wa ligi kuu Uingereza ambapo klabu hizo zinafukuzana kwa sasa.

"Kama Chelsea ingekuwa haijaachwa sana na Man city, basi naamini Chelsea ingeukaribia ubingwa zaidi" alisema Nevin.

Chelsea kwa sasa inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 45 huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi mara baada ya kushushwa jana ambapo mwanzo ilikuwa nafasi ya pili ikishushwa na Manyumbu(Man utd) ambao wao kwa sasa wana alama 47 huku Mama site(Man city) ikiwa kileleni ikiiacha Chelsea kwa alama 14. Na kama Chelsea ikishinda kesho dhidi ya Arsenyani(Arsenal) ambapo kama ikishinda mchezo huo itarudi nafasi yake ya pili.

No comments:

Post a Comment