CHELSEA YAMPATA WA KUCHUKUA NAFASI YA BATSHUAYI - Darajani 1905

CHELSEA YAMPATA WA KUCHUKUA NAFASI YA BATSHUAYI

Share This
Klabu ya Chelsea inajiandaa kupeleka maombi kwaklabu ya Red Star Belgrade ili kumsajili nyota wa klabu hiyo raia wa Ghana, Richmond Boakye ambaye anatazamiwa kutua klabuni Chelsea ili kuweza kuwa mbadala wa Morata endapo atahitajika kutumika na kocha huku mbadala wa sasa wa mshambuliaji huyo, Michy Batshuayi akionekana kutokuwa na chake klabuni hapo huku kukiwa na uwezekano wa kuuzwa au kutolewa kwa mkopo.


Michy Batshuayi anaonekana kushinda kumshawishi kocha Antonio Conte ili atumike na badala yake kocha Antonio Conte anatajwa kumhitaji mshambulijai mwengine wa kuweza kuchukua nafasi ya Batshuayi ambapo sasa anatajwa kumtaka Boakye mwenye miaka 24 ambaye mpaka sasa ameshaichezea klabu yake hiyo michezo 14 na kufunga magoli 15.

Lakini pia Chelsea ilikuwa inatajwa kumuwania mshambuliaji wa Celtic, Moussa Dembele ingawa mpango huo unaonekana kutokuwa katika mwendelezo mzuri.

No comments:

Post a Comment