NYOTA WA WIKI; UNAIKUMBUKA HII YA WILLIAN? - Darajani 1905

NYOTA WA WIKI; UNAIKUMBUKA HII YA WILLIAN?

Share This
Willian amekuwa nyota wa mchezo ambapo Chelsea iliiadhibu Stoke city magoli 5-0, huku mwenyewe akitengeneza magoi na kufunga goli moja kwa mkwaju wa penati. Mara baada ya kuwa nyota wa mchezo huo, nyota huyo kuonyesha mapenzi yake kwa Chelsea, wiki hii amekana kutaka kuondoka klabuni hapo akidai ana furaha na napenda kuendelea kudumu ndani ya klabu hiyo inayopatikana London Magharibi.

Sasa nasi tulimchagua kuwa nyota wa wiki mpaka pale Chelsea itakaposhuka uwanjani kucheza mchezo mwengine ambapo imepangwa kushuka kesho kupambana na Arsenyani(Arsenal) iliyo nyumbani, Emirates.

Leo nataka nikukumbushe kitu ambacho kinamhusu Willian ambaye jina lake kamili ni Willian da Silva Borges ingawa pia kinatuhusu sisi sote tukiwa kama mashabiki wa Chelsea, ila pia kama mashabiki wa mchezo wa soka.

Unakumbuka mwaka juzi yaani mwaka 2016 mwezi Oktoba kilichotokea? Willian alipata taarifa za kumpoteza mama yake aliyekuwa anaugua ugonjwa wa kansa au saratani na alipambania uhai wake dhidi ya ugonjwa huo kwa miaka 2 kabla ya kufariki akiwa na miaka 57.

Baada ya taarifa hizo, Willian aliruhusiwa na klabu kusafiri kwenda kuhudhuria mazishi ya mama yake huko nchini Brazil ambapo kwa wiki hiyo, Chelsea ilikuwa ikijiandaa kucheza mchezo wake dhidi ya Leicester city, na katika mchezo huo, Chelsea ilifanikiwa kushinda 2-0 huku magoli yakifungwa na Diego Costa aliyeshangilia kwa kuweka herufi ya 'W' kwa kutumia vidole vyake akonyesha kumpatia pole mchezaji mwenzake Willian na Eden Hazard nae alifunga katika mchezo huo naye kuonyesha namba 22 kupitia vidole vyake ambapo namba hiyo inavaliwa na Willian akionyesha kumpa pole nyota huyo kutokana na majanga aliyokutana nayo.

Lakini pia mara baada ya mchezo huo kocha Antonio Conte aliuelekeza ushindi huo kwa winga huyo akimpatia pole kwa kupitia kipindi kigumu.

Mara baada ya mazishi kufanyika na kupewa muda wa kupumzika, Willian alirejea klabuni Chelsea na akajiandaa mazoezini kujiandaa na mchezo wa ligi kuu uliopangwa kuchezwa tarehe 31-Desemba-2016 ambapo Chelsea ilitakiwa kupambana na Stoke city, na Willian alihusika katika mchezo huo akifunga magoli mawili kwenye ushindi wa mabao 4-2 huku akionekana kulia katika kushangilia kwake magoli hayo kutokana na kumbukumbu za mama yake.

Unaikumbuka hiyo? Pole sana Willian na Chelsea kwako ni kama familia.

No comments:

Post a Comment