HAZARD AMWAMBIA HAZARD ATAFUTE TIMU NYENGINE - Darajani 1905

HAZARD AMWAMBIA HAZARD ATAFUTE TIMU NYENGINE

Share This
Familia ya winga na mshambuliaji wa Chelsea, Eden Hazard inaangalia uwezekano wa nyota wa klabu hiyo Kylian Hazard ambaye ni mdogo wa Eden Hazard ambaye mwenyewe anaiichezea akademi ya Chelsea kuweza kutafuta klabu nyengine ili aweze kuungana nayo kutokana na kuona kutakuwa na ugumu kwa Kylian kuweza kupata nafasi klabuni hapo ili aje kucheza soka la kulipwa zaidi.



Mzazi wa kinda huyo ambaye ni baba yake mzazi anayeitwa Thierry Hazard alikaririwa akisema hunda wakafanya jitihada ili mtoto wake ajiunge na klabu nyengine tofauti na Chelsea.

Lakini pia leo, mdogo mwengine wa Eden Hazard ambaye alishawai kuwa klabuni Chelsea ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Borrusia Monchnglebach ya nchini Ujerumani inayoshiriki ligi kuu nchini humo, Thorgan Hazard naye amesema "Ingekuwa vyema kwa Kylian(Hazard) atafute klabu nyengine ili aweze kupata mafanikio kwa haraka.

Akademi ya Chelsea imekuwa ikitengeneza vipaji na kuvigundua vipaji mbalimbali lakini mwisho wa siku inaonekana ni ngumu kwao kupata nafasi katika kikosi cha wakubwa huku klabu ikiwatoa kwa mkopo na kusajili nyota wengine kutoka klabu nyengine.

Baadhi ya nyota wa Chelsea waliotokea kwenye akademi ya Chelsea na wengine kuuzwa na kutolewa kwa mkopo ni Ruben Loftus-cheek aliye Crystal Palace kwa mkopo, Jeremie Boga, tammy Abraham akiwa Swansea kwa mkopo huku nathaniel Chalobah akiuzwa Watford, Nathan Ake akiwa klabuni Bournemouth, Betrand Traore aliyeko Olympique Lyon.

No comments:

Post a Comment